Baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini KCCB limetoa wito kwa wakenya kuungana kwa pamoja ili kupiga vita dhidi ya jinamizi la ufisadi nchini.
Baraza hilo chini ya uenyekiti wa askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Kisumu Maurice Muhatia makumba amesema kuwa kuungana kwa wakenya dhidi ya ufisadi ndio njia ya kipekee ya kukomesha ufisadi.
Baraza hilo kadhalika limesisitiza kuwa kanisa katoliki halijakataa usaidizi kutoka kwa wanasiasa Bali linapendekeza kuwa mchango huo kufanywa kwa ukimya bila kutumika kujionyesha