Mama mboga yuko hatarini Nandi

Wafanyibiashara katika eneo la Namgoi wameandamana kulalamikia kile wanasema kuangaishwa na maafisa wa jiji kaunti ya Nandi.

Wafanyibiashara hao wamesema vibanda vyao vimebomolewa na kushinikizwa kuendeleza biashara zao katika soko kuu mjini Kapsabet licha ya wao kudokeza kwamba kwa miaka mingi sasa,wamekuwa wakitegemea biashara hizo ,na hatua ya kubomolewa kwa vibanda vyao,ni kuwarudisha kwa umaskini.

Sasa wanataka serikali kuu kuingilia kati kwa kuwa hawana imani tena na viongozi wao kaunti hiyo kuwanusuru na mwekeleo ambao wanasema wanasukumwa kwa lazima kuingia kwenye umaskini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *