Wauguzi wa hospitali ya mafunzo na Rufaa ya Moi Eldoret wameanza tena mgomo wao kutokana na kile wanasema usimamizi wa hospitali hiyo kudinda kuafikia matakwa yao.
Wakizungumza na wanahabari wakiongozwa na afisa wa uhusiano mwema Beatrice Chelulei,wauguzi hao walidokeza kwamba walikuwa wametoa makataa ya siku ishirini na moja kwa usimamizi la sivyo watasitisha huduma zao swala wanalosema halikuzingatiwa.
Wanalalamikia kupunguzwa kwa mgao uliokuwa umeelekezwa kwa hospitali hiyo kwa shillingi billioni 2.3 wakitaka hatua za haraka kuchukuliwa la sivyo hospitali hiyo huenda ikaanguka.
Wanasisitiza kwamba kamwe hawatarejea kazini hadi pale matakwa yote yatakapotimizwa.
Wanadai kuongezewa mishahara,kupandishwa vyeo miongoni mwa maswala mengine ya kimsingi.