Kanisa katoliki nchini limejiunga na Kanisa la Kianglikana nchini na kuweka msimamo mkali ya kuwakataza na kuwakanya wanasiasa kuhutubu kwenye madhabahu.
Akizungumza wakati wa hafla ya kutawazwa kwa Askofu mwandamizi wa jimbo katoliki la Meru askofu mkuu wa jimbo katoliki la Nyeri Anthony Muheria amesisitiza kwamba kanisa halitatumika kama ulingo wa siasa na kurindima siasa na chuki miongoni mwa viongozi hao.
Kauli ya kanisa katoliki inajiri siku chache baada ya kanisa la kiangalikana likiongzwa na askofu mkuu Jackson Ole Sapit kuwapiga marufuku wanasiasa kuongea kanisani ila wawe waumini kama wanaohudhuria ibada.