Wakristu wametakiwa siku zote kukubali maumbile Yao kwa kuwa Mungu aliwaumba kwa utukufu wake.
Askofu wa jimbo la jeshi Wallace Nganga akihubiri katika Misa ya ufunguzi wa wa warsha ya wanahabari wa vituo vya kanisa katoliki ametoa wito kwa Kila mmoja kusadiki jinsi alivyoumbwa pasi na kutumia kemikali kukosoa maumbile Yao.
Askofu kadhalika ametoa wito kwa Kila mmoja kuwa chombo cha matumanini kwa wale waliokata tamaa kwa kuwakosoa kwa Upendo basi na kuangalia tu makosa Yao.
Ulimwengu ukiadhimisha siku ya wagonjwa duniani askofu Wallace kadhalika ametoa wito kwa Kila mmoja kuombea wagonjwa na kuwapa matumaini pamoja na wale wanaowahudumia