Ndoa chanzo cha familia

Kanisa linapoadhimisha siku ya wanandoa duniani wito umetolewa kwa wanandoa kuhalalisha ndoa yao na kuisalimisha katika kristu kama njia moja ya kupata nguvu na neema ya kukabiliana na changamoto ambazo zinakumba wito huo.

Siku kuu hii husherehekewa kila dominika ya pili ya mwezi wa Februari lengo kuu likiwa ni kuipa hadhi sakramenti ya ndoa ambayo ni kiungo muhimu katika ukuaji wa kanisa Mahalia nyumba ya wote.

Askofu msaidizi wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Simon Peter Kamomoe ametoa wito kwa wakristu kutumia mwaka huu wa jubilee kuhalalisha ndoa zao kanisani akisema kuwa Baraka ambazo mkristu hupata kupitia kwa sakaramenti ya ndoa humjalia mja karama nyingi kutoka kwa mwenyezi Mungu.

Askofu ametoa wito kwa mapadre kote nchini kuwahimiza wanadoa wachanga na kuwafunza zaidi kuhusu wito huo ambayo kwa sasa unakumbwa na changamoto si haba.

Amewataka wazazi kadhalika kuwa kielelezo chema kwa kupalilia mila zilizo njema kwa wanao akisema kuwa kule kutelekeza wajibu wa malezi huenda ikaathiri kwa kiwango kikubwa kizazi kijacho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *