kazi ghushi

Swala la ukosefu wa kazi miongoni mwa mamilioni ya wakenya hasa vijana likizidi kuwa kero,baadhi ya vijana waliojitokeza katika chuo cha kiufundi cha kitaifa cha Eldoret wamekashifu wizara ya Leba kwa kutangaza uwepo wa nafasi hizo kisha kuambulia patupu.

Wakizungumza na wanahabari chuoni humo,vijana hao walisema walitarajia kupata angalau nafasi hizo za kazi ila walivunjika moyo walipoelezwa kwamba hakuna mahojiano kuhusu kazi yoyote licha ya wao kupata habari kupitia mitando ya kijamii kwa nafasi hizo kwenda mataifa mbalimbali za nje ikiwemo taifa la Dubai.

Walisikitikia kile walisema wengi wao wana vyeti vya kufuzu kwenye vitengo mbalimbali ila hakuna nafasi za kazi.

Yanajiri haya baada ya mamia ya vijana kujitokeza kwenye chuo cha Eldoret Polytehcnic kusaka nafasi za kazi kwenda mataifa za nje,baada ya juhudi zao kuambulia patupu licha ya kutolewa kwa notisi ya mahojiano hayo kutoka wizara ya leba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *