Askofu wa jimbo katoliki la Kitale Henry Juma Odonya amebuni maeneo mawili ya kipastorali katika jimbo hilo kama njia moja ya kurahisisha shughuli za uinjilishaji kwa wakristu wa jimbo hilo.
Jimbo hilo sasa litakuwa na maeneo mawili ya kipastorali ya Pokot na eneo la kipastorali la Transnzoia ambapo askofu Juma amemteua padre Mathew Rotich kuwa padre mkuu wa eneo la Pokot huku Moses akiteuliwa kuwa padre mkuu wa eneo la Transnzoia
Askofu Juma kadhalika amefanya mabadiliko katika dekania mbalimbali kufuatia uhamishao wa mapadre kwenda kuhudumu katika parokia zingine jimboni humo.