UGONJWA WA MTRH

Wagonjwa katika hospitali ya Rufaa ya Moi Eldoret wametabika kupata matibabu baada ya wahudumu wa afya hasa madaktari katika eneo la North Rift Kuanza mgomo wao rasmi siku ya jumatano.

Wagonjwa hao kutoka maeneo mbalimbali mwa nchi waliofika katika hospitali ya MTRH wanasema wamesubiri kuhudumiwa hadi wamekata tamaa,huku wakitaka serikali kusikiliza kilio cha madaktari hao ndipo mkenya wa kawaida asipata changamoto za matibabu.

Wakati huo,mwenyekiti wa muungano wa madkatari wa meno,na wanafamasia KMPDU ukanda wa North Rift Kamonzi Mulei amesema hawarudi nyuma hadi serikali iafikia matakwa yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *