Waathiriwa 6,000 Kila mwezi wa ugonjwa wa Saratani

Ugonjwa wa saratani ukiendelea kuorodheshwa kuwa sugu na yenye kuchangia maafa mengi ulimwenguni,watu Zaidi ya 6,000 kila mwezi wanapatikana na ugonjwa huo katika hospitali ya MTRH Eldoret.

Kulingana na afisa mkurugenzi wa hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi Eldoret Philip Kirwa,visa hivi vinaongezeka kila kuchao kutokana na kile wananchi kutambua hali yao ya afya baada ya makali yake kuwa katika kiwango cha juu.

Aidha,afisa huyo amewataka wakenya kujitenga na kasumba ya kuhusisha ugonjwa huo na laana akisema kuna wataalam wa hali ya juu na ambao mgonjwa anapopatikana na saratani atatipiwa kwa wakati ufaao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *