Askofu mkuu wa jimbo katoliki la Nyeri Anthony Muheria ametaka kila mmoja kuwa hujaji wa matumaini.
Askofu Muheria amesema kuwa huu ni wakati wa kila mmoja kujihoji na kuwa tumaini kwa yule ambaye amekata tamaa maishani mwake ambayo kwa sasa inapandashuka nyingi.
Kiongozi huyo wa kidini ametoa wito kwa kila mmoja kujifunga nira ya matumaini kwa kujitwika msalaba wa maisha kwa kuisalimisha msalaba huo kwa mwenyezi mungu kama njia moja ya kupata mapumziko.