Jubilei; Mahujaji wa matumaini wawajibishwa

Mama kanisa anapoadhimisha mwaka wa jubilei wakristu wametakiwa kujikita sana katika maisha ya sakramenti ambayo hujenga agano kati ya mja na muumba wake.

Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nyeri Anthony Muheria, amesema kuwa jubilei ya mwaka huu umejikita katika mwito wa sinodi wa kutembea pamoja kama familia na jamii ya mungu, kwa kushiriki na kusihi maisha ya sakramenti kama tunu msingi ya kujenga uhusiano kati ya mkristu na mwenyezi Mungu.

Amesema kuwa kutakuwa na matukio mbalimbali ya kuadhimisha mwaka wa jubilee, yakiwemo hija katika maeneo mbalimbali, adhimisho la ekaristia takatifu, na hata kushiriki toba na kutenda matendo ya kiutu sanjari na kusali, ili kupata neema kupitia kwa maridhiano na msamaha wa dhambi.

Ikumbukwe kuwa baba mtakatifu Francisko alizindua mwaka wa jubilei mwezi wa desemba mwaka jana, kwa kufungua mlango mtakatifu ambayo utawasaidia wakiristu kutafakari matendo na kauli mbiu ya mwaka huu ambao inawakumbusha kuwa mahujaji wa matumaini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *