Wakristu walio na majukumu mbalimbali katika kanisa wametakiwa kutekeleza kazi yao kwa uadilifu bila kujali vishawishi kutoka kwa wale wanaowatizama kwa njia tofauti.
Askofu wa jimbo la Jeshi Wallace Nganga akihubiri katika misa ya kufuzu kwa walimu wa watoto wa kimisionari kwenye kanisa la queen of apostles Ruaraka jimbo kuu katoliki la Nairobi, ametoa wito kwa walimu hao kutoyumbishwa na masengenyo kutoka kwa wakristu wenzao, bali wamakinikie wito wa kuwatumikia watoto wa kimisionari na kanisa kwa ujumla wake.
Ametoa wito kwa walimu hao kuwa mfano bora kwa watoto hao kwa kuwa wao ndio barua wanaosomwa na watoto wa kimisionari, akiwataka siku zote kuonyesha mfano bora katika kanisa kupitia kwa mienendo, maongezi na mavazi kwa utukufu wa mwenyezi Mungu.
Amewataka kutotegemea malipo katika kazi hiyo, bali wajitolee kumtumikia mwenyezi Mungu bila kujali yale watakaopokea kutoka katika maeneo mbalimbali ya kazi, akisema kuwa amana na Baraka ni kutoka kwa mwenyezi Mungu.