Eldoret ;Watawa wa Benediktini baraka kwa jimbo

Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich amepongeza uwepo wa watawa wa shirika la kibenediktini katika bonde la Kerio, akisema kuwa watawa hao wamekuwa wa msaada mkubwa kwa wahanga wa machafuko na jamii nzima zinazoishi katika eneo hilo.

Akihubiri kwenye misa ya kuadhimisha jubilee ya miaka ishirini na tano ya mtawa Rosa Pascal wa shirikia la kibenediktini kwenye mtaa wa Karen jijini Nairobi, askofu amesema kuwa ujio wa shirika hilo kwenye eneo pana la bonde la Kerio, umekuwa wa manufaa kwa kuwa wamekuwa kimbilio kwa wale waliokata tamaa na hata wale waliohitaji msaada wao.

Askofu Kimengich kadhalika ametoa wito kwa watawa wa shirika hilo kujisadaka bila kujibakisha katika utendakazi wao, kwa kuwapa matumaini wale waliokata tamaa katika maisha, akisema kuwa kujitolea kwao katika huduma za jamii imekuwaa wa manufaa makubwa katika jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *