Jimbo la Eldoret sasa limefika Ulaya

Askofu wa jinbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich amebuni maeneo matatu mapya ya kipsatorali katika mataifa ya kigeni kama njia moja ya kutembea pamoja na wakristu wanaoishi katika mataifa hayo.

Katika waraka wake askofu amesema kuwa kubuniwa kwa maeneo hayo matatu ya kipastorali  yananogeshwa na ruwaza ya sinodi ambayo iliwekwa wakfu jimboni mnamo Aprili mwaka wa 2023, ili kupiga jeki shughuli za uinjilishaji kwa wakristu wazaliwa wa jimbo katoliki la Eldoret wanaoishi katika mataifa hayo ya ughaibuni.

Maeneo ambayo yamebuniwa ni pamoja na North amerika Europe na eneo la kipastorali ya austarilia, askofu akifafanua hii inatokana na utofauti wa majira katika maeneo hayo.

Kadhalika askofu Kimengich amewtwika majukumu mapadre watatu wa kuongoza maeneo hayo matatu, padre Thomas Kigeni akiteuliwa kuongoza eneo la kipastorali la Europe, naye padre Hillary Rotich akiteuliwa kuongoza eneo la kipastorali la Australia  huku padre Ignatuis Kipchirchir akitwikwa jukumu la kuliongoza eneo la North Amerika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *