Mwaka wa Jubilei ukiwa unaadhimishwa,wito umetolewa kwa walimu wanaowasimamia watoto kanisani maarufu Animators kuwasaidia watoto wamishonari hao kuwa na Imani dhabiti katika kristu.
Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Philip Anyolo Subira amesisitiza haja ya walimu hao kuwaongoza vyema watoto wamishonari ili pia wakiwa watu wazima waweze kuendelea kumhubiri huyo kristu.
Wakati huo,askofu mkuu amesisitiza haja ya kila mmoja kuimarisha uhusiano wao na kristu kupitia sala maana hiyo sala ndio inampa nguvu mkristu kupigana na adui.