Baraza la magavana nchini COG limewarai maafisa wa kliniki kusitisha mgomo wao ulioanza rasmi jana likisema kwamba, baadhi ya matakwa yao yanayowafanya kususia kazi yameshughulikiwa.
Kupitia kwa taarifa,COG limisema kwamba,utata huo umetokea baada ya kutoelewana kwenye mkutano uliofanywa juma lililopita na muungano huo hasa kutokana na matakwa mapya yaliyoibuliwa.
Wito huu unatokea wakati na ambapo kulikuwa na mkutano kati ya washikadau wa sekta ya afya ikiongozwa na katibu wa maswala ya huduma ya kijamii katika wizara ya afya Harry Kimtai na maafisa wa mamlaka ya afya ya kijamii SHA na pia magavana.
Johnson Sakaja ni mwenyekiti wa wafanyikazi kwenye baraza la magavana akiwataka wahudumu hao kuitikia mwito wa kurejea kazini
Kwa upande wake, mwenyekiti wa wanakliniki Peterson Wachira amekariri kuwa mgomo bado ungalipo kwani wanasema kwamba serikali imedinda kuafikia mkataba wa maelewano namna ilivyokuwa imeratibiwa.