Bishop Kimengich: Wanasiasa komesheni ubinafsi

Ubabe wa kisiasa ukionekana kuchukua mkondo mwingine nchini,wito umetolewa kwa wanasiasa kukoma kuwa wabinafsi na badala yake kutimiza malengo waliyotoa kwa wananchi.

Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich amesikitikia kile anasema uongozi wa sasa wa kisiasa umejawa na ubinafsi na kutojali wengi swala analosema sharti likome na wanasiasa kuwajibikia utendakazi wao.

Kuhusiana na matamshi aliyotoa aliyekuwa rais Uhuru Kenyatta ya kuwataka vijana kutokubali mali yao iharibiwe,amesisitiza kwamba iwapo wazo lake mstaafu huyo ilikua ya kulinda mali kwa kujieza bila kuharibu mali ya umma unastahili ili kusaidia serikali kupata mwelekeo bora na siyo kukosa heshima na kuwavunjia heshima wengine.

Askofu Kimengich amesema na iwapo kuna nia fiche swala hilo halistahili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *