mitando itatumaliza au itujenge

Wakenya wakionekana kufurahia uhuru wa kujieleza kupitia vyombo vya kijamii,wito umetolewa kwao kuwa makini na semi au hata picha na video wanazotundika kwenye ukurasa zao za mitandao ya kijamii.

Askofu msaidizi wa jimbo katoliki la Eldoret John Lelei amesema japo kuna uhuru huo wa kujieleza kutumia vyombo hivyo,ni vyema kwa wakenya kumakinikia maneno yao ndipo isije ikaweka matatani taifa na kuvuruga Amani iliyopo.

Askofu Lelei amesisitiza kwamba kila mmoja ako na uhuru wa kujieleza ila uhuru huo usihujumiwe kwa kuwakosea wengine heshima.

Ikumbukwe kuwa,yanajiri haya wakati na ambapo kumeshuhudiwa majukwaa ya kijamii yamefurika cheche za matusi na video zisizoridhisha hasa kuwaelekeza wanasiasa swala ambalo limezua tumbo joto ya iwapo inaweza kuvuruga uwiano na utangamano miongoni mwa wakenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *