Biashara haisongi

Wafanyibiashara  wanaouza masanduku ya shule katika jiji la Eldoret kaunti ya Uasin Gishu wamelalamikia biashara zao kurudi chini wakati huu kufuatia utekelezwaji wa mtaala mpya wa elimu ya CBC ambapo sasa hamna wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza ambao walikua wanajiunga na shule za bweni kwa wingi miaka ya hapo awali na hivyo kuinua biashara yao.

Wakizungumza jijini Eldoret walisema kwamba,walitarajia watapata wateja kama miaka iliopita ambapo walikua wakiyauza masanduku mengi sana ya shule kwa wanafunzi lakini hali sasa imekua ngumu kwani,wazazi wengi ambao watoto wao wanajiunga na gredi ya tisa hawawapeleki kujiunga na shule za bweni baada ya serikali kusema wasalie kwenye shule za msingi ambazo wamekua wakisomea.

Aidha, walisema kwamba wateja wachache ambao wanajitokeza wanalalamika ukosefu wa fedha kufuatia hali ilivyo jambo ambalo wanasema linaathiri sana biashara zao na kuwapelekea hata kushindwa kulipa mikopo huku wakisema wana matumainj serikali itaweka mpango wa kuboresha uchumi ili wakenya wasiendelee kuumia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *