Siku Mwizi ni Arobaini

Maafisa wa polisi jijini Eldoret wanawazuilia washukiwa wawili wa wizi wa vifaa vya stima ikiwa ni pamoja na transfoma.

Akithibitisha haya,kamanda wa polisi kaunti ya Uasin Gishu Benjamin Mwanthi alisema kwamba maafisa wa usalama kwa ushirikiano na maafisa kutoka kwa kampuni ya kusambaza umeme KPLC walifanikiwa kuwanasa watu hao katika eneo la Munyaka wakiwa kwa gari ambayo inaaminika wamekua wakitumia kutekeleza wizi wao.

Kamanda huyo alipongeza ushirikiano uliopo kati ya asasi za usalama na wakazi akisema kwamba kamwe hawatalegeza Kamba kupambana na wahalifu hao.

Kwa upande wake,mbunge wa Ainabkoi kaunti ya Uasin Gishu Samwel Chepkonga alilaani visa hivyo akisema zinarejesha nyuma utunzaji na uimarishaji wa miundomsingi mashinani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *