Msalaba wa mkatili wabebeshwa mama

Mahakama moja ya Kapsabet kaunti ya Nandi imeruhusu kuendelea kuzuiliwa kwa mwanamke mmoja aliyekuwa mwakilishi wadi na anayeaminika kuwa mama wa mshukiwa mkuu wa mauaji ya kijana mmoja aliyewaua kikatili katika eneo la Chemase.

Mwili wa marehemu ulipatikana ukiwa bila baadhi ya sehemu za mwili ikiwa ni pamoja na kichwa,vidole na sehemu za siri chanzo cha wakazi wenye hasira kujitokeza na kuvamia kituo cha polisi kisha kumpiga hadi kufa mshukiwa mkuu pamoja na kuzuru boma ya mshukiwa mwingine na kumuangamiza kabla ya kuteketeza gari la polisi katika kituo cha polisi ya Chemase.

Mwanamke huyo Caren Otieno ambaye alisemekana kuwa mamake mshukiwa alikuwa mwakilishi wadi mteule katika eneo la Muhoroni kaunti ya Kisumu na ataendelea kuzuiliwa kwenye kituo cha polisi kwa siku nne zaidi kusaidia maafisa hao kwa uchunguzi.

Akitoa agizo hilo,Hakimu mkuu wa Mahakama ya Kapsabet Kibet Sambu aliwapa nafasi maafisa wa polisi kumzuilia mshukiwa kusaidia kwa uchunguzi hadi tarehe 10 Januari mshukiwa akitarajiwa kufikishwa mahakamani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *