Imani tosha utakujalia maisha ya Mbingu

Askofu wa jimbo katoliki la Ngong’ John Obala Owaa amewataka wakristu kujisadaka bila kujibakisha katika kuimarisha Imani yao kwa kristu.

Kulingana naye,ukristu ni tunu msingi ambao unapaswa kupaliliwa na kulindwa kila muda ndipo wakristu waweze kuridhi ufalme wa mbingu.

Vilevile,askofu Owaa aliwataka watumishi katika shamba la bwana kutumikia miito yao kwa uaminifu na kuwaongoza wakristu katika njia salama za kuingia mbinguni.

Aidha,aliwataka watumishi hao wanapoendelea na shughuli zao za kila siku kuwaongoza wakristu katika njia salama za uzima wa milele,wafanye hivyo bila ubaguzi wowote wa kitabaka,kidini au hata kwa kuwatenga wengine kwa kuwa na kimo tofauti,akieleza kwamba,ufalme wa mbingu ni kwa wote wanaomtambua na kumwamini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *