Wanafunzi wa vyuo vikuu na vya Kadri katika kaunti ya Nandi wamejitokeza na kuomba serikali ya kitaifa kuhakikisha inaongeza mgao wa fedha unaoelekezwa kwa basari ili wasiojiweza katika jamii watimizie ndoto zao.
Wanafunzi hao wakiongozwa na mwenyekiti wao Bernard Lagat ni kwamba,iwapo hatua hiyo itaafikiwa,wanafunzi kutoka familia masikini wataweza kupata masomo na kuafikia malengo yao maishani.
Wakati huo,Lagat aliwataka wanafunzi kujituma kwenye masomo yao hasa yale wanaoyopenda kufanya ili wajiwezeshe kimaisha na pia kujitegemea.