Balozi wa Baba Mtakatifu nchini Kenya Mwadhama Hubertus Mathews Maria van Megen, aliwataka watawa kujisadaka bila kujibakisha kwa kuishi maisha ya utakatifu.
Akihubiri alipoongoza Misa ya kuwapa nadhiri watawa wa shirika la Sisters of Mary of Kakamega katika jimbo la Kakamega,Van Megen aliwataka watawa kutumikia miito yao kwa uaminifu na kwa unyenyekevu.
Wakati uo huo aliwakumbusha kuzingatia nadhiri zao licha ya kwamba baadhi yao kuwa wasomi na wataalam katika Nyanja mbalimbali.