Askofu Kimengich :UTII KWA WITO BARAKA TELE

Askofu wa jimbo Katoliki la Eldoret Dominic Kimengich aliwahimiza mashemasi kuishi maisha ya utakatifu katika huduma yao kwa kanisa na jamii.

Akiongea alipoongoza misa ya daraja la ushemasi kwa waseminaristi 16 katika jimbo Katoliki la Eldoret, askofu Kimengich alielezea umuhimu wa mashemasi hao kuwa mfano bora na kumuiga Kristu katika huduma yao.

Askofu walipongeza kwa uvumilivu wao na kutokata tamaa akiwahimiza kujikaza na kukamilisha safari yao hadi kupewa daraja takatifu la Upadri.

Wakati uo huo askofu Kimengich alipongeza juhudi za mtanguliza wake marehemu askofu Cornelius Korir kwa kukuza miito hali ambayo imechangia kuengezeka kwa idadi ya mapadre na watawa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *