mkasa wa moto

Wakazi wa mtaa wa Jerusalem viungani mwa jiji wa Eldoret katika kaunti ya Uasin Gishu wanakadiria hasara ya zaidi ya shilingi milioni moja baada ya nyumba zao za makazi na biashara zao kuteketea kwenye mkasa wa moto hii leo asubuhi.

Inadaiwa kwamba moto huo ulizuka majira ya saa kumi na moja za alfajiri kutoka kwa hoteli moja kabla ya kusambaa kwa haraka na kuteketeza hoteli,maduka na nyumba za watu za kuishi ambazo zilikua zimejengwa kwa mabati na mbao.
Wapangaji wa nyumba hizo wakiwemo wanafunzi wanadai kupoteza stakabadhi muhimu za masomo kwenye moto huo 

Akithibitisha haya kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya moiben Stephen Okal alisema kwamba hakuna mtu aliyejeruhiwa kwenye mkasa huo lakini polisi wanaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *