Wito umetolewa kwa walimu wa vijana wa kikundi cha kati cha watoto wamishonari kanisa katoliki maarufu MYM kuhakikisha kwamba wanasaidia vijana hao kukuza imani yao kwa kuwaweka karibu nao kila wakati.
Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Eldoret John Lelei liwataka walimu hao kuhakikisha kwamba wanatambua pandashuka na changamoto amabzo vijana hao wanapitia ili kuwasadia kimaadili na pia kuwasaidia kukuza imani.
Wakati huo,askofu Lelei alisisitiza haja ya kikundi hicho kuwa na heshimu iwe wakubwa au wadogo ndipo ujana wao usiwe wa kukwaza ila ya kutegemewa na kuheshimiwa pia.