Jimbo katoliki la Eldoret limeaandaa hafla ya tatu ya kila mwaka ya ‘dhifa ya askofu’ (Bishop’s Dinner) kwa lengo la kukusanya fedha za kusaidia na kuendeleza miradi mbalimbali katika jimbo.
Kupitia kwa kamati andalizi, dhifa ya mwaka huu inanuia kuchangisha fedha za kusaidia mradi wa ujenzi wa kituo cha vijana (Pacem In Terris) eneo la Biretwo parokia ya Emsea kaunti ya Elgeiyo Marakwet.
Moira Chepkok ni mwenyekiti wa kamati andalizi akiwashukuru wakristu na wahisani wambao wamechangia kwa namna mbalimbali kufanikisha malengo ya dhifa hiyo.
Padre msimamizi wa idara ya vijana jimboni Jonas Kiplimo anaelezea zaidi kuhusu mradi wa Pacem In Terris.
Vilevile kituo hicho kinanuia kuwa na majengo kadhaa ikiwemo Adoration Chapel, bweni, ukumbi wa mikutano na kadhalika.
Askofu Dominic Kimengich na msaidizi wake askofu John Lelei wanatarajiwa kuongoza dhifa hiyo ambayo itahudhuriwa na wakristu kutoka parokia mbalimbali wakiwemo wageni waalikwa.