Mwalimu wa dini kiungo muhimu katika kanisa kwa kuwa wao ndio hupamba Sherehe za kiliturjia.
Askofu msaidizi wa jimbo katoliki la Eldoret John Kiplimo Lelei akihubiri katika Misa ya Kila mwaka wa walimu wa dini ametoa wito kwa walimu hao siku zote kuwashirikisha wakristu na kuwa kiunganishi kati Yao na kristu.
Ametoa wito kwa makatekista daima kutotosheka tu na kuwa mwalimu Bali wawe na ufahamu Zaidi kwa kuwa wao ndio waelekezi akisema kuwa kule kufahamu ndio kutawawezesha kukosoa Zaidi.
Askofu Lelei amewataka makatekista kushirikiana na mapadre na viongozi wengine wa kanisa ili kupiga jeki uinjilishaji.