Chuo kingali mahame

Matumaini ya kufunguliwa kwa chuo kikuu cha Moi-Eldoret yanaendelea kudidimia baada ya wafanyikazi wa chuo hicho kusisitiza msimamo wao kwamba hawatarejea kazini hadi matakwa yao yatimizwe kikamilifu.

Hatma ya wanafunzi kufuzu na wengine kukamilisha masomo yao haijulikani huku wahadhiri wa chuo hicho wakiendeleza mgomo wao ambao umedumu zaidi ya mwezi mmoja.

Wahadhiri wameelezea mahangaiko wanayopitia chuoni humo huku makato yao kwenye mishahara ikikosa kuwasilishwa kwa taasisi husika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *