Viongozi wa kidini katika kaunti ya Nandi sasa wanataka viongozi wale waliochangia kutiwa saini kwa mkataba wa maelewano na kampuni ya Adani kuchunguzwa na idara ya ufisadi EACC ili haki itendeke kwa wakenya.
Wakizungumza mjini Kapsabet,viongozi hao wamesema kwamba yastahili kwa waliosimamia hatua hiyo kuchunguzwa ili fedha za umma isije ikawa imefujwa.
Vilevile,viongozi hao walisema kwamba hatua aliyochuka rais William Ruto kusimamisha kabisa kmapuni ya Adani kutekeleza ukarabati kwenye uwanja wa kimataifa JKIA na pia kampuni ya kusambaza umeme KETRACO ni afueni kwa wafanyikazi wa makampuni hizo kwani wanasema wangepoteza ajira.
INSERT ONE ADANI NANDI
Kadhalika,viongozi hao walisema kwamba rais aliwasikiza wakenya na hatua hiyo ni njia moja ya kurejesha Imani kwa wakenya.