wagema wako taabani

Maafisa wa utawala katika kaunti ya Nandi wamefanikiwa kunasa pombe haramu Zaidi ya lita mia mbili katika kijiji cha Kamurguywo eneo bunge ya Aldai.

Akithibitisha haya,chifu eneo la Kamurguywo Emily Kurgat alisema kwamba walifanikiwa kupata pombe hiyo kufuatia ushirkiano wake pamoja na maafisa wanaopambana na biashara hiyo katika eneo hilo linaloaminika kuwa kitovu cha biashara hiyo haramu.

Kurgat ameongeza aidha kwamba,pombe hiyo usafirishwa kutoka kaunti Jirani eneo la Magharibi mwa nchi akisisitiza kwamba maafisa wa utawala hawatalegeza kamba kukabiliana na wafanyibiashara wanaoendelea na biashara hiyo.

Chifu huyo alilalamikia uwepo wa pombe hiyo kuwa chanzo kuu cha kudorora kwa afya na hata kwa familia nyingi kuyumba kwa kuwa wanafamilia hawawajibikia majukumu yao,kutokana na unywaji na biashara ya pombe haramu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *