Wito umetolewa kwa wakristu kujisadaka bila kujibakisha katika safari ya Imani kwa kuwa Imani huyo huja na karama nyingi kutoka kwa mwenyezi Mungu.
Kwa mujibu wa askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Kisumu Morris Muhatia Makumba alisisitiza haja ya makleri na majandokasisi kuwa waaminifu kwenye utumishi wao katika shamba la bwana.
Askofu mkuu Muhatia Vilevile,aliwataka watumishi hao na kila mmoja kumakinikia miito yao maishani ili waweze kupata karama zake mwenyezi mungu.
Wakati huo,askofu Muhatia alisisitiza haja ya watumishi katika shamba la bwana kuwaongoza vyema wakristu katika maisha ya unyofu wa moyo.