Sinodi kwa Wote

Askofu mkuu wa jimbo Katoliki la Nyeri Anthony Muheria aliwataka wakristu kutumia mitando ya kijamii kwa njia inastahili hasa katika uenezwaji wa injili.

akizungumza kwa njia ya video baada ya kukamilika kwa kongamano la sinodi huko Roma,alitaka kanisa kuishi maisha ya Ubatizo na kama wakristu kwa kwa kuhusisha wote.

Askofu Muheria vilevile,aliwataka wakristu kutumia zawadi na talanata walizojaliwa ipasavyo na kuwajali wengine maishani mwao.

wakati huo,askofu mkuu Muheria aliwataka wakenya kuishi kwa pamoja na amani iweze kudumu kwa kile anasema kanisa linategemea kila mmoja .

yanajiri haya wakati na ambapo,askofu Mkuu Muheria amekuwa Roma pamoja na askofu mkuu Martin Kivuva Musonde kama washiriki kwenye kongamano la maaskofu wakatoliki nchini Kenya wa Sinodi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *