Wito umetolewa kwa wananchi kukoma kununa dawa za kupunguza makali katika maduka ya dawa bila ushauri wa Daktari kwa kuwa hulka hiyo umechangia uharibifu wa viungo mwilini, na kusababisha ongezeko la visa vya maafa yanayosababishwa na Antimicrobial Resistance Drugs.
Kulingana na daktari Paul Olale afisa wa afya katika shirika la Msalaba Mwekundu,watu wengi wana mazoea ya kuzuru maduka ya dawa na kujitafutia dawa hizo bila maelekezo ya madaktari swala analosema,likiendelea watu zaidi ya millioni 10 duniani watakua wameaga kutokana na hulka hiyo.
Vilevile,afisa huyo amesema kwamba wakulima wengi hutumia dawa hizo za kupunguza maumivu almaarufu antimicrobials katika mashamba yao ili kurutubisha mimea au hata kuwapa mifugo yao, swala analosema limechangia kwa mwili wa binadamu kukosa kustahimili dawa mtu apougua na hata kukosa kupona na badala yake huongeza hata magonjwa.
Kwa upande,mratibu wa shirika la Msalaba Mwekundu Kaunti za Uasin Gishu na Nandi Alice Njari amesema kwamba wameshirikiana na washikadau mbalimbali kutoa hamsisho kwa umma kuhusiana na matumizi na athari za antimicrobials.