Mshukiwa mkuu wa mauaji ya mwanamme anayeaminika kuwa mumewe kwa kumpiga risasi mara kumi na mbili ,ameeleza mahakama ya Eldoret kwamba alikuwa anajaribu kujitetea kwa mumewe anayesema alikuwa anataka kumpokonya bundiki lake.
Mbele ya Jaji wa mahakama Kuu ya Eldoret Reuben Nyakundi ,mtuhumiwa huyo Konstable Lilian Biwott ameliambia mahakama kwamba, anakumbuka vyema wakati wa tukio hilo ikiwa ni Oktoba 14 2023 ambapo alimpata mumewe akiwa kwenye chumba chao cha kulala na kisu mkononi,wakati wa tukio akiwa anatoka kazini na amebeba bunduki lake.
Mwanamke huyo anasema hapo awali, alimsikia mumewe Victor Kipkemboi dereva wa Matatu na baba wa watoto wawili akipiga simu kwa mtu ambaye hakumfahamu kwamba, atawaua wanao na alipokuja jioni hiyo naye chumbani humo, waliweza kutofautiana kabla ya kumuua mumewe wakinganngania bunduki lake,akiongeza kwamba huenda marehemu angemuua kabla yake kujitetea kwa kufyatua risasi.
Aliambia mahakama kwamba,mumewe amekua akimdhulumu mara si moja.
Kesi hiyo itaendelea kususikilizwa mnamo Oktoba tisa mwaka huu kabla ya kesi hiyo kufungwa, huku mshukiwa akiendelea kuzuiliwa kwenye gereza la Wanawake la Gk Eldoret.