first choice mataatani tena

Waathiriwa wa sakata ya uajiri ughaibuni kupitia kampuni ya First Choice wameandamana jijini Eldoret kwa mara nyingine wakitaka kukamatwa kwa wakala wa kampuni hiyo Judith Jepchirchir.


Wananchi hao kutoka maeneo mbalimbali kuanzia kaunti za Trans-nzoia,Kericho na maeneo mbalimbali nchini wamejitokeza na kutaka idara ya kushughulikia mashtaka ya umma kuingilia kati na kusaidia kutiwa mbaroni kwa wakala huyo.


Wamesikitikia kile wanasema kukosa kupata haki kutokana baadhi ya maafisa wa usalama ambao wamezembea kazini na kudai kuwa anashirikiana na wakala huyo  na hata  kukosa kumkamata.
Sasa wameapa kuchukua Sheria mkononi mwao na kumkamata wakala huyo iwapo matakawa Yao hayatasikilizwa.


Kwa upande wake,mwanaharakati wa shirika la Center against Torture Kimutai Kirui alitaka asasi za usalama kuwajibikia utendekazi wao na kutowabagua wananchi wanaotafuta haki.


Ikumbukwe kuwa,malalamishi haya yanakuja wakati na ambapo waziri wa  ilisitisha utendekazi wa kampuni ya First Choice kutokana na malalamishi ya kuendelesha biashara ya utapeli,huku kesi dhidi ya kampuni hiyo ikiwa inaendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *