Kina mama na vijana wamehimizwa kutoyumbishwa na madhehebu mbalimbali yanayochipuka kwa sasa ambayo nia yao ni kuwapotosha na kuwatapeli.
Askofu wa jimbo katoliki Henri Juma Odonya akihubiri katika misa ya kuwatawaza kina mama wakatoliki cwa jimboni humo ametoa wito kwa kila mmoja kutambua imani yao kikamilifu akisema kuwa hiyo ndio njia moja tu itakayomwezesha kila mmoja kusimama imara kiimani.
Ametoa wito kwa vijana kadhalika kamwe kutopumbazwa na utajiri wa haraka kwa kuwa tama hupelekea vijana hao kujiingiza katika visa vinavyokinzana na maadili na halkadhalika kupelekea wao kupoteza maisha yao.
Amewahimiza kila wakati kutembea na Mungu kwa kusikiliza sauti yake ili siku zote neno hilo liaongoze kkatika vita dhidi ya maovu yanayokabili dunia kwa sasa.