Walimu wa kwaya na watunzi wa nyimbo wametakiwa kutunga nyimbo ambazo zimenogeshwa na liturjia.
Askofu wa jimbo katoliki la Ngong John Oballa Owaa akihubiri katika Misa iliyowaleta pamoja wanakwaya jimboni humo, ametoa wito kwa walimu wa kwaya kujitenga na nyimbo za tamaduni na kuangazia nyimbo za roho mtakatifu, ili kuelekeza nyoyo za wakristu kwake mwenyezi Mungu.
Ametoa wito kwa wanakwaya kadhalika kuwa mfano Bora kwa wakristu akitoa wito kwao kujitenga na kutumbuiza waumini kanisani, na badala yake waimbe nyimbo ambazo zinateka nyoyo za waumini na kuwasaidia kutafakari neno la Mungu.
Askofu Oballa ametoa wito kwa wanakwaya kuungana pamoja kwa kuangazia maadili,
kama vile kuwa tayari kujifunza, kuzingatia mavazi na kukumbatia wengine kwa
Upendo Wala sio kueneza chuki.