ASKOFU DOMINIC:Ufisadi jinamizi kuu

Baba mtakatifu Francisko ametoa wito kwa baraza nzima la maaskofu wa kanisa katoliki nchini KCCB kuimarisha vita dhidi ya jinamizi la ufisadi nchini.

Huu ni ujumbe wake Baba Mtakatifu katika ziara ya baraza hilo mjini Vatican alamaarufu AD limina ambapo ametaka baraza hilo kuimarisha vita dhidi ya janga hilo kwa  kutoa sauti kukemea visa vya ulaji rushwa, kuhamasisha jamii kuhusu athari za jinamizi la ufisadi, akisema kuwa taifa la Kenya linawezaimarika kiuchumu iwapo swala hilo litakabiliwa ipasavyo.

Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominik Kimengich aliyekuwa katika ziara hiyo amesema kuwa bara la afrika, taifa la Kenya likiwa miongoni mwa mataifa ambayo yamekumbwa na athari za ufisadi linastahili kutilia maanani vita hivyo na kuweka mikakati kabambe ya kukomesha hulka ya hongo miongoni mwa visa vingine vya ufisadi iwe katika ngazi ya serikali au katika jamii, askofu Kimengich akisema  kuwa baraza hilo la KCCB limeweka mikakati ambayo itajadiliwa kwenye baraza kuu ili kutathmini mbinu zaidi akitoa wito kwa kila mmoja kushirikiana katika vita dhidi ya janga hilo.

Kadhalika swala uinjilishaji hapa nchini haikusazwa maaskofu wakitakiwa kuwashirikisha kiukamilifu mapadre katika majimbo yao ili kupambana na maswala ibuka ambayo huenda yakayumbisha imani yakiwemo teknolojia, mabadiliko ya tabianchi na ekolojia fungamani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *