Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich ametoa wito kwa wanasiasa kukoma kurindima ngoma za uchaguzi mkuu ujao na badala yake wawahudumie wakenya.
Askofu Kimengich amesema kuwa huu si wakati wa kupandisha joto la kisiasa akitaka wanasiasa wote nchini kukumbatia uwiano maridhiano kwa faida ya mshikamano wa kitaifa.
Kulingana naye,siasa ambazo zinashuhudiwa kwa sasa huenda zikazamisha taifa hili kwenye shimo la umaskini.
Askofu Kimengich aliwataka wakenya kushirikiana na kujituma katika shughuli zao za kila siku ili kukomesha wao kutegemea sana serikali kwa misaada ya kila wakati.
Vilevile,askofu Kimengich alilaumu swala la ufisadi ambalo anasema limechangia mno kukithiri kwa misukosuko katika taifa hili akiwataka wakenya kujitenga na ulaji wa rushwa na hongo.
Aidha,askofu Kimengich aliwataka wazazi kuwa mstari wa mbele kuwaelekeza wanao akiashiria kuwa visa vingi vya ufisadi nchini imechangiwa na mafunzo na malezi duni ya wazazi.