Jimbo lapata mapadre manyanga

Mapadre wapya wametakiwa kujisadaka bila kujibakisha kama njia moja ya kupiga jeki shughuli za uinjilishaji.

Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich akihubiri katika Misa ya Daraja la upadirisho ya mashemasi nane jimboni ,ametoa wito kwa mapadre hao kumakinikia wito waliotikia akisema kuwa huo ni wito kutoka kwa mwenyezi na kamwe wasiyumbishwe na mambo ya Dunia hii.

Ametoa wito kwa wakristu siku zote kuendelea kuwaombea na kuombea miito mbalimbali haswa wito akisema kuwa, huu ni wito ambao una changamoto na kupitia kwa uaminifu na Sala ndio itakayowaongoza kupigana na changamoto hizo.

Askofu Kimengich amewahimiza wakristu kuzidi kuombea miito akisema kuwa jimbo linatarajiwa kuwapa Daraja la ushemasi waseminaristi kumi na sita mwakani.

Kutokana na ongezeko la wale wanojitokeza kuitikia wito wa utawa askofu anasema kuwa jimbo linapania kuanzisha chuo cha kipekee cha kukuza wito huo wa upadre.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *