Makleri na majandokasisi wametakiwa kushirikiana katika shughuli za uinjilishaji kama njia moja kuonyesha wakristu ramani ya kwenda mbinguni.
Askofu wa jimbo katoliki la Kitui Joseph Mwongela aliwataka makleri hao, kushirikiana na kunyenyekea akisema kuwa wito waliochagua ni karama kutoka kwa mwenyezi Mungu ambao utawawezesha kuurithi ufalme wa mbingu.
Hata hivyo,askofu Mwongela aliwatahadharisha wakristu dhidi ya kuona makosa na kuwahukumu wengine akisema kuwa mkristu anastahili kumrekebisha mwenzake kwa upendo kila anapoteleza.