Wito umetolewa kwa wakristu kuhakikisha wanatumia simu kwa njia inayostahili isije ikasambaratisha familia zao.
Askofu wa jimbo katoliki la Nakuru Cleophas Oseso Tuka aliwatahadharisha sana wakristu wasiwe watumwa wa simu,akisema kuwa,vifaa hivyo vimewafanya wengi wao kusahau matumizi yake.
Askofu Tuka alisisitiza kwamba,simu hizo zastahili kutumiwa tu wakati mwafaka ili kuwaepusha wakristu kuzamisha maarifa yao kwenye simu na kukosa kuwa wabunifu.
Wakati huo,askofu Tuka aliwataka walimu wa dini kuangazia upya mafundisho yao kwa wanafunzi wao wasiwe wanapitwa na wakati wa ujio wa maswala mapya katika jamii kwa hili,akisema itakuwa mwongozo tosha kuwawezesha wanafunzi wao na maarifa zaidi ya kidini.