Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Philip Anyolo Subira amewataka makleri na majandokasisi kutumikia miito yao kwa uaminifu.
Kulingana naye, alisema ipo haja ya wakristu siku zote kumakinikia neno la Mungu akisema kuwa neno hilo ndilo litakalowabadilisha kimawazo na halkadhalika kuwapa mwelekeo.
Askofu Anyolo hata hivyo alitoa wito kwa makleri hao kuwaelekeza wakristu ipasavyo kwa na kuwaheshimu kama njia moja ya kukuza hadhi yao kama wakristu.