Jeshi kukabidhiwa askofu mpya Oktoba

Monsinyori Wallace Nganga atasimikwa kama askofu wa tatu wa jimbo la jeshi tarehe Kumi na mbili mwezi wa kumi mwaka huu.

Hii ni kufuatia kuteuliwa kwa Monsinyori Wallace kuteuliwa na baba mtakatifu Francisko tarehe Kumi na tano mwezi agosti kuwa mchungaji wa jimbo Hilo la jeshi baada ya kusalia chini ya usimamizi wa Monsinyori Benjamin Maswili na John Njue baada ya Aliyekuwa mchungaji wa jimbo Hilo Alfred Rotich kustaafu.

Hadi kuteuliwa kwake Monsinyori Wallace Nganga amekuwa akihudumu kama askofu msaidizi wa jimbo kuu katoliki la Nairobi ambapo amehuduma kwa miezi nane baada ya kuteuliwa kuwa askofu msaidizi.

Ikumbukwe kuwa, jimbo la jeshi lilibuniwa na Baba mtakatifu Yohane Paulo wa pili tarehe ishirini na nane mwezi wa Saba mwaka wa 1981 huku askofu wa kwanza wa jimbo Hilo akiwa Maurice Kadinali Otunga akifuatwa na askofu Alfred Rotich ambaye kwa Sasa ni mchungaji wa jimbo katoliki la kericho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *