Mwanamume mwenye umri wa miaka 48 amekamatwa kwa tuhuma za kumwuua mwanawe wa miaka 24 katika eneo la Mosombecho kaunti ya Nandi.
Inaarifiwa kuwa mwanamume huyo alimdunga mwanawe kwa kisu mara kadhaa na kupelekea kifo chake katika hospitali ya rufaa ya Kapsabet.
Ripoti ya polisi inasema kuwa mwendazake alidungwa mara kadhaa kifuani kufuatia mzozo wa kinyumbani na babake.
Mwili wake umehifadhiwa katika makafani ya hospitali ya Kapsabet ukisubiri kufanyiwa upasuaji.