Wakaazi wa eneo la Matisi kaunti ya Trans-Nzoia waliokuwa walitoa ardhi yao kupisha ujenzi wa barabara kuu ya Kitale-kuelekea taifa la Uganda wamelalamikia kuchelewesha kwa malipo waliyokuwa wameahidiwa.
Wakizungumza katika eneo hilo,wakaazi hao walisema maagano yao na serikali imekiukwa ikizingatiwa kuwa walikuwa wametoa ardhi yao kwa ujenzi wa barabara hiyo kuu.
Wenyeji hao ambao maduka yao yalibomolewa walitaka halmashauri ya barabara kuu ya Kenha kuwalipa ridhaa yao kama walivyokubaliana miaka miwili iliyopita wakati ujenzi wa barabara hiyo ilipoanza.