Komesheni mgomo

Washikadau kutoka sekta ya elimu kaunti ya Nandi waliwataka walimu chini ya muungano wa walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri Kuppet kusitisha mgomo wao na kuruhusu mazungumzo na serikali.

Wakiongozwa na mwanzilishi wa Kampuni ya ufadhili ya Hokil Zaccious Rop walisema kwamba mgomo unaathiri masomo ya wanafunzi ikizingatiwa ni muhula wa tatu wenye kuwavukisha wanafunzi darasa lingine ifikapo mwaka ujao.

Alisema yastahili chama cha walimu iwapo wanamaliliyo yoyote waweze kuwasilisha kwa serikali au taasisi husika kwa muda mwafaka ili kupunguza athari za kuathirika kwa masomo.

Yanajiri haya wakati na ambapo Kuppet ilisema itaendelea na mgomo hadi matakwa yao yatatutiliwe hii ni licha ya mahakama ya leba Jijini Nairobi hapo jana kupitia kwa jaji James Rika kusimamisha mgomo wa Kuppet kufuatia kesi iliyowasilisha na TSC,mahakama ikiwataka walimu hao kurejea kazini hadi kesi hiyo isikizwe Septemba tano.

Mgomo huu unajiri wakati shule zimefunguliwa kwa muhula wa tatu ambapo watahiniwa wa darasa la nane na kidato cha nne wakitarajiwa kufanya mitihani yao ya kitaifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *